Friday, 13 July 2018

Clement Sanga Wa Yanga Avuliwa Uenyekiti Bodi ya Ligi (TPLB) Baada ya Yanga Kudai Bado Wanamtambua Yusuf Manji

Kikao cha Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kilichofanyika jana Julai 12,2018,  makao makuu ya shirikisho hilo, kimemuondoa  aliyekuwa mwenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPLB), Clement Sanga,  kwenye nafasi hiyo kwa kukosa sifa baada ya klabu ya Young Africans kuthibitisha Yusuph Manji kuwa ndiye mwenyekiti wa klabu hiyo.

Wakati huohuo, Kamati ya Uchaguzi  ya TFF imeelekezwa kuandaa uchaguzi wa kuziba nafasi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo Uwanja wa Karume mjini Dar es Salaam, Rais wa shirikisho hilo, Wallace Karia,  alisema  hatua hiyo imefuatia mkutano wa Juni 10 wa wanachama wa Yanga ambao ulitamka kuwa bado unamtambua Yussuf Manji kama Mwenyekiti wao.

Pia, Kamati ya Utendaji ya TFF imemthibitisha Wilfred Kidao kuwa Katibu Mkuu wa shirikisho hilo.

No comments:

Post a Comment