Wednesday, 6 June 2018

Nafeli sana katika Menejimenti – Enock Bella

Msanii Enock Bella amedai kinachopelekea ngoma zake kutosikika kwa sana ni kutokana na kukosa menejimenti ya uhakika.
Kauli ya muimbaji huyo inakuja mara baada ya kuachana na menejimeti iliyokuwa inamsimamia kutoka nchini Uganda.
“Mara nyingi kinachonifelisha kama Enock ni kuwa active katika kazi zake kwa sababu ya menejimenti ninazozipata mara nyingi huwa mbovu,” amesema.
“Yaani nafesli sana katika menejimenti lakini nikipata menejimenti inayojitambua nakujua muziki ni nini na dhamani ya msanii ipo wapi wanaweza wakashangaa Watanzania,” Enock ameiambia Wasafi Tv.
Ameendelea kwa kusema ana idadi kubwa ya nyimbo ambazo zipo ndani na ameimba tofauti kabisa na vile ambavyo amezoeleka ila hazisikiki kutokana hana menejimenti nzuri ya kusimamia hilo. Hivi karibuni Enock ameachia wimbo mpya uitwao Kurumbembe.

No comments:

Post a Comment