Friday, 1 June 2018

Msanii wa Bongo Flava, Ruby amefunguka kuhusu kuhusisha muziki wake na masuala ya kushirikina.

Msanii wa Bongo Flava, Ruby amefunguka kuhusu kuhusisha muziki wake na masuala ya kushirikina.

Muimbaji huyo anatayetamba na ngoma ‘Niwaze’ katika mahojiano na Papaso, TBC FM amesema kwa upande wake ni kitu ambacho hakifahamu kabisa.
“Siko hivyo na wala sijawahi, mimi nina bibi yangu, nina babu yangu wapo Tanga na ndio nyumbani kwetu hayo mengine siyajui,” amesema Ruby.
Ameendelea kwa kusema kuwa siri ya mafanikio ni Mungu, kufanya muziki mzuri, kuwapenda mashabiki wake na aina ya watu ambao ameamua kufanya nao kazi.

No comments:

Post a comment