Sunday, 10 June 2018

Matukio mbalimbali katika Mahafali ya Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu Uvccm Mkoa wa Arusha

Naibu Katibu Mkuu wa Ccm Bara Ndg.Rodrick Mpogolo Akimkabidhi hati ya Pongezi Mwenyekiti wa Vijana wa Ccm Mkoa wa Arusha Saitoti Zelothe katika Mahafali ya Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu UVCCM yaliyofanyika katika ukumbi wa Naura Spring Hotel Arusha.
 Baadhi ya  Wahitimu wa Idara ya Vyuo na Vyuo vikuu UVCCM Mkoa wa Arusha wakikabidhiwa vyeti vya pongezi na Mgeni Rasmi ndg:Rodrick Mpogolo katika Sherehe za Mahafali ya kuwaaga Makada wa CCM idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu uvccm Mkoani hapa.
 Kaimu Katibu Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu UVCCM Taifa Ndg Daniel Zenda Akiteta jambo na Mwenyekiti wa Vijana wa Ccm Mkoa wa Arusha Saitoti Zelothe.


Naibu Katibu Mkuu wa Ccm Ndg. Rodrick Mpogolo Akiwakabidhi kadi wanachama wapya.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Ccm Mkoani Arusha Ndg. Loota Sanare Akizungumza katika Sherehe za Mahafali ya kuwaaga Makada wa CCM idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu uvccm Mkoa wa Arusha.
Meza Kuu wakiburudika na nyimbo ya CCM.


 Baadhi ya Wahitimu wakimsikiliza kwa Makini Naibu Katibu Mkuu wa Ccm Bara Rodrick Mpogolo hayupo pichani.
Mwenyekiti wa Uccm Mkoa wa Arusha Saitoti Zelothe Akifurahia jambo wakati wa Mwenyekiti wa Ccm Mkoa wa Arusha Ndg.Loota sanare Alipokuwa anahutubia wahitimu.
Kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Arumeru Ndg.Timotheo Mnzava  Akibadilishana mawazo na Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha Mjini Ndg.David Mwakiposa.
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg. Athumani Kihamia Akifuatilia kwa makini Risala ya Wahitimu.
Katibu Hamasa wa Vijana Mko wa Arusha Ndg. Omary Lumato Akimsisitizia jambo Katibu Tawala wa Wilaya ya Arumeru Ndg.Timotheo Mnzava.
Katibu Hamasa wa Wilaya ya Arusha Mjini Ndg. Mutu Marijani Akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa vijana kata ya kati ambaye pia ni  mjumbe wa baraza kuu la mkoa la vijana Ndg. Jamila.
Kutoka kulia  ni Mwenezi wa Jiji la Arusha Ndg.Abrahamu Mollel Akikaribishwa ukumbini kwenye Mahafali ya vyuo na vyuo vikuu yaliyofanyika leo Jijini Arusha katika Ukumbi wa Naura Spring Arusha.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Arumeru Ndg. Timotheo Mnzava akishangilia jambo katika Sherehe za Mahafali ya kuwaaga Makada wa CCM idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu uvccm Mkoa wa Arusha.
Kutoka kulia  ni  Katibu wa Vijana wa Ccm Mkoa wa Arusha  Ndg. Saidi  Goha Akishauriana jambo na Katibu Hamasa wa Vijana Mkoa Ndg. Omary Lumato.
Baadhi ya Wahitimu Jenipher Isaya Ambaye ni Makamu wa Rais kutoka Chuo cha Arusha University Akifuatiwa na Anitha Rweyemamu Mjumbe kutoka Chuo cha Uhasibu Arusha pamoja na Justice Nyagali ambaye ni Katibu Hamasa wa Chuo cha Mount Meru University.

No comments:

Post a Comment