Halmashauri ya Wilaya ya Meru imeibuka mshindi wa jumla katika mashindano ya umoja wa michezo ya Shule za Sekondari (UMISSETA) kwenye mkoa wa Arusha  na kupata vikombe vya ushindi 5 kati ya michezo 7 iliyoshindaniwa.

Michezo hiyo ya (UMISSETA) iliyofanyika kwa siku tano kuanzia Mei 26 hadi 30/2018 Mkoani Arusha ambapo Halmashauri saba za Mkoa wa Arusha zilishiriki mashindano hayo ambapo Halmashauri ya Meru ilishinda michezo mingi na kuwa mshindi wa jumla Kimkoa kwa kushika nafasi ya mshindi wa kwanza katika michezo ya  mpira wa kikapu (basketball) kwa wavulana, mpira wa mikono (Handball)wavulana na fani za ndani (indoor games) ,pia ilishika nafasi ya pili kwenye michezo ya mpira wa kikapu (Basketball)kwa wasichana pamoja na mpira wa wavu (volleyball )kwa wavulana .

Miongoni mwa wachezaji wa Timu mbalimbali za Halmashauri ya Meru zilizoshiriki mashindano haya ya UMISSETA wamesema  sababu za wao kushinda ni nia ya kushinda waliyokuwa nayo iliwafanya kuwa na Ushirikiano na nidhamu na wameishukuru Halmashauri ya Meru kwa uratibu mzuri uliofanyika kwenye ngazi ya Wilaya.
Aidha wachezaji hao wameenda mbali zaidi kwa kuomba muda wa maandalizi  kuongezwa ili kuwawezesha wachezaji kufanya mazoezi ya kutosha.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Christopher Kazeri amewapongeza wachezaji walioshiriki mashindano hayo ya UMISSETA pamoja na viongozi kwa kufanya vizuri na kufafanua kuwa Halmashauri ya Meru inatambua umuhimu wa Sekta ya michezo na itazidi kuboresha mambo mbalimbali kwenye Michezo.

Naye Afisa michezo kwenye Halmashauri ya Meru Aimbora Nnko ametoa wito kwa jamii na wadau mbalimbali wa michezo kuvitunza na kuviboresha viwanja vya michezo vilivyopo kwenye maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Meru kwani michezo inafaida nyingi ikiwemo ajira na uboreshaji wa afya .
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilya ya Meru Christopher J. Kazeri akipokea mojawapo ya Kikombe cha ushindi wa mashindano ya michezo UMISSETA ngazi ya Mkoa  toka kwa Kaimu afisa Elimu Sekondari Abedinego Mulokozi,ambapo Halmashauri yake ilikuwa mshindi wa kwanza kati ya Halmashauri saba za mkoa wa Arusha zilizoshiriki.
Picha ya pamoja ya Wakuu wa idara na Vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru  na watumishi wasiowakuu wakuu waidara/vitengo wakiwa kwenye picha ya pamoja ya kufurahia ushindi wa Halmashauri hiyo kwenye mashindano ya UMISSENTA.
Afisa elimu Sekondari kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru  Mwl.Damari Mchome (aliyetumia ishara ya mkono) pamoja na viongozi wa wachezaji walioshiriki mashindano ya UMISSETA ngazi ya Mkoa
Picha ya pamoja ya baadhi ya Wachezaji wa mchezo wa mpira wa kikapu (basketball) kwa wavulana, mpira wa mikono (Handball)wavulana na fani za ndani (indoor games) ,pia ilishika nafasi ya pili kwenye michezo ya mpira wa kikapu (Basketball)kwa wasichana pamoja na mpira wa wavu (volleyball )kwa wavulana  wa walioibuka washindi wa kwanza kwenye mashindano ya UMISSETA mkoa wa Arusha 
Picha ya pamoja ya baadhi ya Wachezaji wa mchezo wa mpira wa mikono (Handball)wavulana  walioibuka washindi wa kwanza kwenye mashindano ya UMISSETA mkoa wa Arusha 
Picha ya pamoja ya baadhi ya Wachezaji wa mchezo wa fani za ndani (indoor games) wa walioibuka washindi wa kwanza katika mashindano ya UMISSETA mkoa wa Arusha 
Picha ya pamoja ya baadhi ya Wachezaji wa mchezo wa mpira wa kikapu (basketball) kwa wasichana walioibuka washindi wa pili kwenye mashindano ya UMISSETA mkoa wa Arusha 
Picha ya pamoja ya baadhi ya Wachezaji wa mchezo wa mpira wa  mpira wa wavu (volleyball )kwa wavulana  wa walioibuka washindi wa pili kwenye mashindano ya UMISSETA mkoa wa Arusha 
Picha ya pamoja ya baadhi ya Wachezaji wa timu za mpira wa kikapu (basketball) kwa wavulana, mpira wa mikono (Handball)wavulana , fani za ndani (indoor games) ,mpira wa kikapu (Basketball)kwa wasichana pamoja na mpira wa wavu (volleyball )kwa wavulana zilizopata ushindi wa Jumla kwenye mashindano ya  UMISSETA ngazi ya Mkoa.
Picha ya pamoja ya Wakuu wa idara na Vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru  na watumishi wasiowakuu wakuu waidara/vitengo wakiwa kwenye picha ya pamoja ya kufurahia ushindi wa Halmashauri hiyo kwenye mashindano ya UMISSETA.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: