Tuesday, 29 May 2018

Zaidi ya Wananchi 100 Walala nje ya kituo cha polisi Tarime


Na Clonel Mwegendao,

Wananchi wa Kijiji cha Nkerege wilayani Tarime ambao ni wafuata nyayo za mifugo iliyoibiwa wamejitokeza na kuweka kambi ya kulala ya siku moja katika kituo cha polisi wilayani Tarime kwa madai ya kushinikiza jeshi la polisi kanda maalumu Tarime na Rorya kuwapatia mifugo yao baada ya kufanikiwa kukamata Baadhi ya mifugo na wanaodaiwa kuwa wezi wa mifugo hiyo.

Wimbi la mifugo katika wilaya Tarime bado ni tatizo katika wilaya hiyo ambapo wananchi wameweza kuanzisha nguvu ya pamoja ya kufuata nyayo ili kubaini weze wa mifugo hiyo , akizungumza nje ya kituo cha polisi Tarime kwa niaba ya wananchi hao mmoja wa wafuata nyayo anaeleza kilichowasukuma kuweka kambi na kulala katika kituo cha polisi mjini Tarime ni kuonyesha ushirikiano kwa jeshi hilo juu ya uthibiti wa wizi wa mifugo

Akithibitisha kushikiliwa kwa mifugo ya wananchi hao ambao wamefika katika kituo cha polisi , Hassan Maya ni mkuu wa polisi kitengo cha upelelezi na makosa ya jinai mkoa wa kipolisi Tarime na Rorya Hassani Maya amesema kuwa bado wanaendelea na taratibu zote za msingi ili kuhakikisha watuhumiwa wanachukuliwa hatua stahiki na wananchi wanapata haki yao ya msingi huku akifurahishwa naushirikiano waliouonyesha wananchi hao

Awali akizungumza na wananchi hao kamanda nje ya kituo cha polisi kamnda wa polisi kanda maalumu Tarime na Rorya Hennry Mwaibambe hakusita kuwataka wananchi hao kuacha kuvunja sheria za nchi kwa kudai haki zao bali watumia njia sahihi zinazotii sheria za nchi.

Jumla ya Mifugo minne aina ya Ng'ombe wameweza kukamatwa ambapo wananchi wa kijiji cha nkerege waliweza kuibiwa Ng'ombe wanane.

No comments:

Post a comment