Sunday, 6 May 2018

Yanga wasema haya kuhusiana na hali yao kiuchumi


Uongozi wa Yanga kupitia kwa Msemaji wake, Dismas Teni, umeeleza kwa msisitizo kuwa ni kweli unapitia wakati mgumu hivi baada ya kuyumba kuyumba kiuchumi.

Ten ametoa kauli hiyo wakati akizungumzia maandalizi kuelekea mchezo wao wa leo dhidi ya USM katika Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger huko Algeria.

Ofisa huyo wa Habari amesema Yanga hivi sasa ina tatizo la kuyumba kiuchumi, huku akieleza kuwa ni timu nyingi huwa zinapitia changamoto kama hizo na akiamini siku moja suala hilo litapita.

Yanga imekuwa haina matokeo mazuri msimu katika ligi na mashindano ya kimataifa ukilingana na msimu mmoja nyuma, sababu za kuyumba kwa uchumi zinaelezwa kuchangia pia kikosi kutokuwa imara.

Katika mchezo wa leo wa Kombe la Shirikisho, Yanga itakuwa inawakosa wachezaji wake kadhaa walio mhimili wa kikosi cha kwanza.

No comments:

Post a Comment