Friday, 25 May 2018

Yanga walitufanyia dhuluma, hata nipewe hela zote na BoT siwezi kuwa msemaji wao-Haji Manara

Afisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara amedai kuwa kamwe haitatokea yeye kuihama klabu yake na kujiunga  Yanga SC.
Related image
Haji Manara
Manara amesema kuwa hata kama angepewa fedha zote nchini na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kamwe hawezi kuwa msemaji wa klabu ya Yanga au hata kuwa mwanachama wa klabu hiyo.
Hata kama nipewe hela zote na Benki kuu ya Tanzania (BoT) siwezi kuwa msemaji wa Yanga“. amesema Haji Manara kwenye kipindi cha Maisha Mseto cha Times FM.

Kwa upande mwingine, Manara amesema kuwa kipindi kigumu wanachopitia Yanga kwa sasa ni laana ya dhuluma waliyokuwa wanafanya miaka ya nyuma wakati wa enzi za aliyekuwa Rais wa TFF, Jamal Malinzi.
Yanga walitufanyia dhuluma msimu uliopita kupitia kwa malinzi wao. Dhuluma hiyo inawatafuna mpaka leo. Mafuriko yako kwao, njaa iko kwao, dhuluma hiyo inawatafuna tu.“amesema Manara.

No comments:

Post a comment