Friday, 4 May 2018

Waziri Ndalichako Apinga Walimu Wakuu Kusimamishwa Kazi Kisa Matokeo Mabovu


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako, amewajia juu baadhi ya watumishi wa serikali ambao wanatabia ya kuwafukuza kazi walimu wakuu wa shule ambao hutoa matokeo mabaya katika mitihani ya Taifa.

==>> Unaweza Kuidownload << kwa Kubofya Hapa>>

Ndalichako alisema hayo wakati akijibu hoja za wabunge kuhusu bajeti ya wizara yake na kuongeza watumishi hao hasa maofisa elimu, wanajukumu la kusimamia elimu katika eneo husika na sio kuwatupia lawama walimu pindi matokeo yanapokua mabaya.

“Hiyo sio sawa ni uonevu kwa wakuu wa shule kwa sababu na wenyewe wana viongozi juu yao, kwa nini wao ambao wanatakiwa kuwasimamia wasiwajibishwe, ninaagiza maofisa elimu wafanye kazi yao vizuri, utakuta mtu ana shule tano unashindwaje kuzisimamia, kwa hiyo katika hili serikali itahakiksha tunaimarisha usimamizi ikiwa ni pamoja na kuondoa viongozi ambao ni mizigo”alisema Ndalichako

Ndalichako aliongeza kwamba kama serikali inachukua hatua kubwa ili kuimarisha ubora wa elimu lakini baadhi ya watendaji hao wamekua wakirudisha nyuma jitihada hizo na serikali haitasita kuchukua hatua kwa watendaji hao.

No comments:

Post a comment