Wednesday, 16 May 2018

Waziri Mpina ajibu ishu ya kukamatwa Lori lenye mizogaWaziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina alisimama Bungeni Dodoma leo May 16, 2018 kujibu mwongozo uliotolewa na Mbunge wa Mbinga Mjini Sixtus Mapunda aliyehoji kwamba kuna taarifa mitandaoni kwamba kuna nyama zinauzwa katika machinjio na mabucha zikiwa ni vibudu.

“Tukio hilo lililuwa na jaribio hilo lililuwa ni kinyume cha sheria, baada ya tukio hilo tulichukua hatua ikiwemo kufunga machinjio hayo pamoja na kuagiza mwenye machinjio hayo kukamatwa pamoja na mmiliki wa Lori ambaye tayari amekamatwa” alisema Mpina

“Nataka niwaambie watanzania kwamba tunao usimamizi wa kutosha katika kusimamia usalama kwa walaji wa nyama hivyo wasiwe na mashaka wala hofu nyama za Tanzania ni bora na tunasimamia vizuri wote wanaojaribu kuharibu halii hii tunawachukulia hatua” –Luhaga Mpina

No comments:

Post a comment