Wanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Oldonyosambu wameanza kutumia chumba cha maabara ya somo la Kemia mara baada ya ukarabati wa chumba hicho kukamilika.
Wanafunzi hao wa kidato cha nne, kama walivyokutwana mwandishi wetu, wakifanya jaribio la kuchanganya kemikali kwenye  moja ya Maabara ya somo la Kemia huku wakionekana na nyuso za uhakika wa kile wanachokifanya.
Wanafunzi hao wamekiri kuridhishwa na ukarabati wa maabara tatu za masomo ya Kemia, Fizikia na Biolojia kwa kuwa,  ukarabati huo umewawezesha kufanya majaribio kwa kujiamini zaidi tofauti na hapo awali kabla ya ukarabati huo kufanyika. 
" Tumefurahishwa na ukarabati wa maabara za masomo yote ya Sayansi, kwani maabara hizi zinatuwezesha kufanya majaribio kwa ufasaha huku tukiwa na uhakika wa matokeo wa jaribio tumalolifanya" wamesema wanafunzi hao.
Mkuu wa shule ya Oldonyosambu, mwalimu Leshai Moita, amesema kuwa, jumla ya vyumba vitatu vya Maabara za masomo ya Fizikia, Kemia na Biolojia zimefanyiwa ukarabati kwa mara ya kwanza tangu ilipojengwa 2006 na kufanikiwa kubadilisha miundo mbinu ya maji na gasi.
Mwalimu Moita meongeza kuwa, shule hiyo ya Oldonyosambu ina jumla ya wanafunzi 836, huku wanafunzi 79 wa kidato cha tatu na cha nne wamejiunga na mchepuo wa sayansi na  wanafunzi 473 wa kidato cha cha pili wakisoma masomo hayo ya Sayansi.
Hata hivyo mkuu huyo wa shule amefafanua kuwa, uwepo wa maabara hizo, umeongeza hamasa kwa wanafunzi kuchukua mchepuo wa masomo ya Sayansi  kwani idadi ya wanafunzi inaongezeka mwaka hadi mwaka.
Ongezeko hilo la idadi ya wanafunzi linakwenda sambamba na ufaulu wa wanafunzi katika maso hayo licha ya changamoto ya walimu uhaba wa walimu wa masomo ya Biologia, Fisikia na Hisabati.
Aidha Mkuu huyu wa shule ameendelea kusema kuwa maabara hizo zimekamilika baada ya kufanyiwa ukarabati na kwa kutumia fedha za serikali kupitia mradi wa EP4R, ukarabati uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 15.
Maabara za shule  za sekondari zimekarabatiwa kwa gharama ya shilingi milioni  144.2 zimetumika Serikali kupitia mradi wa Lipa kutokana na matokeo -payment for result (P4R)
Share To:

msumbanews

Post A Comment: