Tuesday, 29 May 2018

Vitu nisivyovipenda kwenye maisha ya muziki ni kuishi kwa skendo – Abdul Kiba

Msanii wa muziki, Abdu Kiba, amesema maisha yake ya muziki hayasukumwi na skendo za mitandao ya kijaami kama baadhi ya wasanii wengine.
Kiba alisema wasanii wengi wanaopenda skendo hawajiamini na wao ndio chanzo cha kushusha thamani ya muziki nchini.
“Muziki ni maisha yangu na kazi inayonipa fedha za kujikimu mimi na familia yangu, napenda kutoa kazi zenye viwango ndio maana mashabiki wananipenda na kuendelea kufuatilia kazi zangu,” Abdul Kiba aliliambia gazeti la Mtanzania.
Aliongeza, “Katika vitu nisivyovipenda kwenye maisha ya muziki ni kuishi kwa skendo, mambo kama haya huwa ni sababu ya kushusha thamani ya mtu na kazi yake,”
Muimbaji huyo mwezi mmoja uliopita alifunga ndoa kufuata nyayo na kaka yake Alikiba.

No comments:

Post a comment