Monday, 21 May 2018

Trump amvaa Obama, ataka FBI ichunguzwe Kama Iliingilia Kampeni Zake

Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa anahitaji uchunguzi ufanyike ili kubaini kama shirika la upelelezi la FBI lilijipenyeza kuchunguza kampeni zake kwa maslahi ya kisiasa.

Trump amesema kuwa anahitaji kujua kama mtangulizi wake rais Barrack Obama aliagiza kufanyika kwa uchunguzi katika kampeni zake.

Ombi hilo limekuja mara baada ya Gazeti la New York Times lilipochapisha taarifa iliyodai kuwa FBI walituma mtu wao kufuatilia mwenendo wa kampeni za Trump mara tu walipopata taarifa za uwezekano wa Urusi kuingilia uchaguzi huo.

Hata hivyo, vyombo vya kisheria vimegoma kutoa ushahidi wa majina ya maofisa waliohusika katika uchunguzi huo kwa kuhofia usalama wao.

No comments:

Post a comment