Monday, 14 May 2018

Tazama picha za matukio mbalimbali yaliyojiri bungeni leo May 14, 2018

Kikao cha 28, mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeendelea Bungeni mjini Dodoma muda huu, likiwa limeongozwa na Mwenyekiti wa Bunge,Najma Giga, ambapo kipindi cha maswali na majibu kimeaendelea; Tazama matukio katika picha

Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Najma Giga akiongoza kikao cha ishirini na nane cha mkutano wa 11 leo Jijini Dodoma

Viongozi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt.Florens Turuka na Naibu Katibu Mkuu Bi.Immaculate Ngwale pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Jenerali Venance Mabeyo wakati wa kikao cha ishirini na nane cha mkutano wa 11 leo Jijini Dodoma

Wachezaji wa Timu ya Simba ambao pia ni mabingwa wa ligi kuu Bara kwa mwaka 2017/18 wakifuatilia shughuli mbalimbali za Bunge leo Jijini Dodoma kwa mualiko maalum wa Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Job Ndugai

Viongozi wa Timu ya Simba wakifuatilia shughuli mbalimbali za Bunge leo Jijini Dodoma kwa mualiko maalumu wa Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Job Ndugai

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.January Makamba akitolea ufafanuzi hoja mbalimbali za wabunge kuhusu changamoto za Muungano wakati wa kikao cha ishirini na nane cha mkutano wa 11 leo Jijini Dodoma

Majenerali wastaafu wa Jeshi la Wananchi watanzania(JWTZ) wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni Jijini Dodoma

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.Dkt.Hussein Mwinyi akiwasilisha hotuba ya Makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

No comments:

Post a Comment