Friday, 18 May 2018

Simba kukabidhiwa kombe na Rais Magufuli, RC Makonda atoa ombi kwa wakazi wa Dar

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewataka wakazi wa jiji hili kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wa Simba dhidi ya Kagera Sugar ambao utahudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.
Makonda amesema kuwa kwenye mchezo huo ambao Simba watakabiziwa kombe lao la ligi kuu itakuwa mara ya kwanza kwake kama Mkuu wa Mkoa na Serikali hii ya awamu ya tano kumshuhudia Rais akishiriki michezo.
Leo tumekutana kwasababu yamambo makubwa mawili, moja ninatimu nyingi katika Mkoa mbazo zimeshiriki katika hii ligi yetu lakini tunafahamu sote Simba ndiyo inakwenda kutwaa ushindi na kesho inakabiziwa kombe kwahiyo nikiwa kama Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na kombe kubaki katika timu ya Wanamsimbazi kwangu mimi ni furaha kubwa na nifahari kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam.
Jambo la pili kubwa ni kwamba kwa uongozi wetu wa TFF ambao uliomba kumualika Mh Rais kuwa mgeni rasmi  taarifa walizotupatia ni kwamba kesho Mh. Rais atakuwa mgeni rasmi katika uwanja wetu wa taifa kushuhudia mechi ya Kagera Sugar na ndugu zetu Simba lakini katika kilele na kukabiziwa kwa kombe, kwahiyo nimeona ni jambo kubwa ambalo kwanza halijawahi kutokea nikiwa Mkuu wa Mkoa lakini pia katika Serikali yetu ya awamu ya tano kumpata Rais anaeshiriki michezo ni jambo moja kubwa sana.
Wekundu wa msimbazi Simba wametwaa ubingwa huu mara ya mwisho ikiwa ni msimu wa mwaka 2011/12 kisha Yanga msimu wa mwaka 2012/13 na Azam FC mwaka 2013/14 kisha Yanga ikatwaa tena mfululizo msimu wa mwaka 2014/15, 2015/16 na 2016/17 na sasa vijana wa Simba wanasema Simba yao, mwaka wao.

No comments:

Post a comment