Tuesday, 29 May 2018

Rubby :Wasanii wamekosa akili ya ziada ya kibiashara

Msanii wa Bongo Flava, Ruby amesema kuwa wasanii wameshindwa kufanya biashara ya muziki kutokana na kushindwa kujitengenezea soko lao binafsi.

Ruby amesema hayo wakati akieleza sababu za ukimya wake kwenye muziki.
“Kwa sababu napenda vitu vizuri na vyenye kukaa kwenye biashara yangu muda mrefu kwa sababu nilikuwa natengeneza soko langu binafsi,” amesema.
“Watu wamekosa ile akili ya ziada ya kibiashara kwamba muziki si vile watu wanataka ila ni vile unautengeza kwa sababu ni kitu chanko kila mtu ana biashara yake,” Ruby ameiambia Clouds TV.
Ruby kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Niwaze ambao amewashirikisha kundi la The Mafik. Huu ni wimbo wake wa kwanza kutoa tangu alipomaliza tofauti zake na Clouds Media January 26, 2018.

No comments:

Post a comment