Friday, 11 May 2018

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Makumira ajinyonga


Mwanafunzi wa mwaka wa pili Chuo Kikuu cha Makumira mkoani Arusha, Luciana Richard (25), mkazi wa Morogoro amejinyonga akiwa chumbani kwake kwa  kile kinachodaiwa kuwa ni msongo wa mawazo.


==>> Unaweza Kuidownload << kwa Kubofya Hapa>>


Tukio hilo limetokea juzi, Kitongoji cha Kilalanaiti Kijiji cha  Ndatu Kata ya pori, mwanafunzi huyo, alikutwa akiwa amejinyonga kwa kutumia mtandio wake alioufunga juu ya mlango wa bafuni.

Akizungumza na Msumba News Blog leo Mei 10, Mwenyekiti wa kijiji hicho, Elisante Pallangyo amesema, mwanafunzi huyo alijinyonga juzi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Yusuph Ilembo amethibitisha jana kutokea kwa tukio hilo na kueleza uchunguzi bado unaendelea.

"Ni kweli tukio limetokea na uchunguzi unaendelea kujua sababu za kujiua mwanafunzi huyu,"amesema.No comments:

Post a Comment