Monday, 28 May 2018

Mkuu wa Mkoa Afungua milango ya uwekezaji


MKUU wa mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka, amefungua milango kwa wawekezaji wa ndani na nje ya mkoa wake kuja kuwekeza na kuongoza fursa za uzalishaji mali kwa wananchi wa mkoa huo.

Mtaka alisema hayo juzi wakati akifungua washa ya siku moja iliyoandaliwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ya kikao kazi cha wanahabari kuhusu uhamasishaji wa sheria ya chakula na dawa, vipodozi na vifaa tiba.

“Nafungua milango ya wawekezaji wafanyabiashara kuja kuwekeza hapa kwa sababu mkoa una amani ya kutosha,” alisema Mtaka.Paia aliwataka watumishi wa mamlaka ya chakula na dawa kutoa ushirikiano kwa vyombo vya habari, ili kutangaza mamlaka na kazi zake huku wakielimisha jamii juu ya matumizi sahihi ya chakula na dawa, vipodozi halali na vilivyopigwa marufuku na serikali ambavyo havifai kwa matumizi ya binadamu, mimea na wanyama.

No comments:

Post a comment