Sunday, 27 May 2018

Mkemi ajiuzulu nafasi zake zote YangaInaelezwa kuwa Mjumbe wa Kamti ya Utendaji ndani ya ya Yanga, Salum Mkemi, amejiuzulu nafasi zake zote ndani ya klabu hiyo.

Taarifa zinazoelezwa zinadai kuwa Mkemi amefikia hatua hiyo kutokana na mashabiki wa Yanga kudai kuwa yeye ni mmoja wa wanaoihujumu Yanga ambayo inayumba kiuchumi hivi sasa.

Hivi karibuni baadhi ya mashabiki wa timu hiyo wamekuwa wakimuandama mjumbe huyo wakidai kuwa anaisaliti timu kwa wakieleza amekuwa akineemeka wakati klabu inaelekea pabaya.

Mashabiki hao wamefikia uamuzi wa kwenda mpaka na mabango Uwanjani wakimuomba Mkemi ajiuzulu pamoja na baadhi ya viongozi wengine walio kwenye Kamati hiyo ya Utendaji.

Licha ya taarifa hizi kuenea, uongozi wa Yanga haujaweka wazi kuhusiana na Mkemi kujivua wadhifa Yanga lakini habari za ndani kutoka klabu hiyo zinaeleza tayari ameshajiondoa ili kupunguza malalamiko ya baadhi ya watu ambao hawamtaki.

No comments:

Post a comment