Monday, 7 May 2018

Mbunge wa CCM Amwaga mamilioni ya fedha kwa kina Mama

Mbunge wa Singida Magharibi Mh: Elibariki Kingu Ametoa zaidi yaSh.{ 7 } milioni kwa ajili ya kuviimarisha kiuchumi Vikundi  7  vya kina mama  jimboni humo kama mitaji isiyo na marejesho. 


Pia, Mbunge huyo ameahidi kutoa msaada wa baiskeli 1530 kwa Mabalozi wote wa nyumba kumi katika Jimbo la Singida Mashariki  zenye thamani ya Sh Milioni mia moja themanini na tatu na laki sita { 183,600,000 } kama moja ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo katika jimbo hilo.

Pia Mh: Kingu Ameahidi mwishoni mwa mwezi wa huu wa tano Ataanza  kusamabaza madaftari na kalamu kwa kila shule zote  za Sekondari katika Jimbo lake,sambamba na hapo Mbunge Kingu ameahidi kugawa vyerehani { 10 } kwa kila Kata ambapo Jimbo la Singida Magharibi lina kata kumi na tano { 15 }

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi fedha hizo jana, Kingu alisema lengo ni kuwajengea wananchi uwezo kiuchumi kupitia mikopo midogomidogo na ujasiriamali.
“Huu ni utekelezaji wa ahadi zangu za kampeni ya kuanzisha na kusaidia vikundi vya maendeleo Kingu ,” alisema.

 Mbunge wa Singida Magharibi Mh:Elibariki Kingu Akimkabidhi Mwenyekiti wa  Kikundi cha  Puma kinachojishughulisha na uuzaji wa mboga mboga Shilingi Milioni Moja Kama moja ya Ahadi yake.
 Kikundi cha Mama Lishe Kikikabidhiwa Fedha ya kujiendesha Sh. Laki Tano kutoka kwa Mbunge wao Mh: Kingu.
Mbunge Kingu Akiwakabidhi  Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ikungi Wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Wilaya Ndg: Mika Likapakapa  fedha kwa Ajili ya Ujenzi wa Ofisi ya chama Wilaya.
Mbunge Akikabidhi fedha kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya Kwaya  Yerusaleem katika  kanisa la KKKT usharika wa Ihanja.
Mwenyekiti wa kikundi cha Kina mama washonaji katika kijiji cha Iseke Akikabidhiwa fedha taslim tsh. Laki tano kutoka kwa Mbunge.

Mbunge wa Singida Magharibi Mh:Kingu akisalimia baadhi ya kina mama ambao ni wajasiriamali wadogo wadogo katika Kijiji cha Puma wakati akielekea kwenye mkutano wa Hadhra katika kata ya Iseke.
Mwananchi wa Kijiji cha Iseke Akimpongeza Mh: Mbunge kwa Utendaji kazi wake uliotukuka .
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Singida  Dokta : Denis Nyiraha Akisisitiza jambo kwenye mkutano wa hadhara wa Mh: Mbunge.
Mbunge Kingu Akihutubia mkutano wa hadhara wananchi wa kata ya Iseke .

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ikungi Ndg: Mika Likapakapa akisisitiza jambo kwa Mh: Kingu  kabla ya kumkaribisha kuhutubia.


 Mzee Mjasiriamali Akimkabidhi muheshimiwa Mbunge zawadi ya miti ya matunda .

No comments:

Post a Comment