Saturday, 12 May 2018

Manara awaomba Bodi ya Ligi wamruhusu kufanya jambo hili leo

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano katika klabu ya Simba, Haji Manara, amefunguka kwa kueleza kuwa atawapigia simu bodi ya ligi ya TFF ili wamruhusu ashangilie leo.

Manara amesema hayo kufuatia kupewa onyo la kungia Uwanjani na kuanza kushangilia baada ya mchezo uliopita dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga uliofanyika Uwanja wa Taifa Aprili 29 2018.

Mkuu huyo wa Idara ya Habari Simba, ameeleza atafanya hivyo ili furaha yake isipotee kwa maana itakuwa ngumu kujizuia endapo Simba itapata matokeo dhidi ya Singida United.

Simba itakuwa ugenini kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida kukipiga na walima alizeti hao walio na kumbukumbu ya kufungwa bao 4-0 kwenye mechi ya awali kwenye mzunguko wa kwanza.

No comments:

Post a comment