Friday, 11 May 2018

Mambosasa: Mange Kimambi Ni Mwenzetu Sasa Hivi,amerudi Kundini Na Anatupongeza

Kamanda wa Kanda maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa ametoa wito kwa vijana kuacha ushabiki bila kuchunguza madhara yake.

Kamanda Mambosasa ameyasema hayo mapema leo wakati akizungumza na wanahabari Jijini Dar es Salaam ambapo amesema mnamo Aprili 26, 2018 Jeshi la Polisi liliwakamata vijana ambao walikuwa kwenye maandalizi ya maandamano ambayo yalihamasishwa kwa njia ya mtandao na mwanadada Mange Kimambi lakini baada ya muda mfupi alianza kuipongeza serikali.

"Nawasihi vijana mnaotumia mitandao ya kijamii mnaposhabikia vitu angalieni madhara, yani faida na hasara zake kwani mnamo Aprili 26 tuliwakamata vijana waliokuwa wakijiandaa kwa maandamano ambapo mhamasishaji Mange Kimambi baadae akaanza kuipongeza Serikali. Mange ameendelea kuipongeza serikali nasi tunampongeza kwa kuwa amerudi kundini", amesema Mambosasa na kuongeza;

"Mange alikuwa anapotosha ila watanzania walipompuuza sasa ametambua ni afadhali naye arudi kuipongeza serikali. Watu tuliowakamata kwa ajili ya kufanya maandamano tuliwahoji na kisha kuwapa dhamana".

Sanjari na hayo Mambosasa amesema kuwa hali ya usalama Jijini Dar es Salaam imezidi kuimarika siku hadi siku

No comments:

Post a Comment