Wednesday, 2 May 2018

MAAJABU YA GARI LILILOTUMBUKIA MTONI!

AMA kweli Mungu mkubwa! Dada mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, amepata ajali kufuatia gari lake aina ya Toyota Prado lenye namba za usajili T435 DED kuacha njia na kutumbukia kwenye mto unaokatiza barabara inayotoka Goba Njia Panda Nne kwenda Madale jijini Dar.

Ajali hiyo ilitokea asubuhi ya Mei 1, mwaka huu na kuwashangaza wapita njia ambao waliona ni maajabu kwa gari hilo kutumbukia kisha mdada huyo aliyekuwemo kutoka akiwa mzima kisha gari kuharibika kidogo tu sehemu ya mbele.

Hata hivyo, baada ya muda trafiki alifika na gari hilo lilitolewa mtoni hapo huku mdada aliyekuwa ndani yake akikataa kuongea lolote.

No comments:

Post a comment