Monday, 7 May 2018

Kitila Mkumbo atii agizo la Rais Magufuli


Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo, ametekeleza kwa vitendo agizo alilopewa na Rais Magufuli, la kwenda kijijini Tundu, Wilayani Mikumi kushughulikia kero ya mradi wa maji kijijini hapo.

Mei 4 mwaka huu akiwa kwenye ziara yake Mkoani Morogoro, Rais Magufuli alibaini kero ya Mkandarasi kuchukua fedha kisha kushindwa kukamilisha mradi wa maji katika kijiji cha Tundu Kata ya Kidodi, ambapo moja kwa moja alimpigia simu Prof. Mkumbo na kumtaka kufika kijijini hapo.

Mei 5, Katibu Mkuu huyo wa Wizara hiyo alifika kijijini hapo na kutatua kero hiyo ambapo tayari marekebisho ya mradi huo yameanza. Mradi huo ulielezwa kukamilika lakini ukashindwa kutoa maji kama ilivyokuwa imepangwa.

Pia Prof. Mkumbo ameunda timu maalum ya watalaam watakaopitia upya usanifu wa mradi huo na kuchukua hatua stahiki kwa wahandisi na mtaalam mshauri aliyesanifu mradi huo.

Mbali na hayo pia Katibu ametoa namba maalum kwaajili ya kurahisisha mawasiliano kwa wananchi wenye kero za Maji waweze kuwasiliana naye moja kwa moja ili aweze kushughulika na kero zao.

No comments:

Post a comment