Tuesday, 29 May 2018

Hii ndio nchi ambayo Prince Harry na mkewe Meghan watapumzika kwaajili ya ‘Honey Moon’

Wakati Dunia nzima ikisubiri kwa hamu kujua sehemu watakayofanyia Fungate (Honey Moon) wanandoa wa familia ya kifalme, Prince Harry na mkewe Meghan Markle hatimaye kitendawili hicho kimeteguliwa.

Kwa mujibu wa watu wa karibu wa familia hiyo ya Kifalme waliohojiwa na mtandao wa TMZ wameeleza kuwa wawili hao wataenda nchini Canada kwa ajili ya fungate.

Taarifa hizo zinakuja baada ya mvutano wa muda mrefu kuwa ni wapi wawili hao wataenda kupumzika baada ya kufunga ndoa huku mitandao mingi ikizitaja nchi za Afrika.

Mtandao wa TMZ pia umeeleza kuwa tayari wawili hao watafikia katika Hoteli ya kifahari ya Alberta’s Fairmont Jasper Park Lodge, ambapo bei ya Chumba (Outlook Cabin) ni Dola za $6,000/=  sawa na tsh Milioni 12 kwa usiku Mmoja.

Hii sio mara ya kwanza kwa familia hiyo ya Kifalme kufikia kwenye hoteli hiyo ya Kifahari kwani mwaka 2005 Malkia Elizabeth II na Prince Philip walifanyia Honey Moon kwenye Hoteli hiyo

No comments:

Post a comment