Thursday, 31 May 2018

Chemical: Sipendi Kutumia kinga (kondomu)


Mwanamuziki anayefanya poa na ngoma zake , Chemical ameweka wazi kuwa yeye siyo muumini wa kutumia kinga (kondomu) ndiyo maana mara nyingi anapenda kuwa kwenye mahusiano na mtu ambaye ni muaminifu.

Kupitia kipindi cha Kikaangoni  kinachorushwa na EATV, Chemical amesema hayo wakati alipoulizwa na mtangazaji wa kipindi hicho mara yake ya mwisho kutumia kinga.

"Mara ya mwisho kutumia kinga wakati nafanya mapenzi ni muda kidogo, ila kiukweli mimi sio shabiki wa kinga kabisa. Mambo ya kinga kinga mimi hapana ndiyo maana napenda sana kuwa na mtu aliyetulia."-  Chemical

Pamoja na hayo Msanii  huyo ameweka wazi kwa sasa hayupo kwenye mahusiano na mtu yoyote kwa kuwa ameamua kuchagua kutengeneza maisha yake na kuhofia kuumizwa moyo wake

No comments:

Post a comment