Bunge
limebadilisha ratiba ili kuruhusu waumini wa dini ya Kiislamu kushiriki
kikamilifu mfungo mtukufu wa Ramadhan bila kuathiri shughuli za chombo
hicho cha Dola.
Utenguaji
wa kanuni hizo umefanywa bungeni leo Jumatano Mei 16, 2018 na Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama na kuungwa mkono na wabunge.
Kwa
mujibu wa Mhagama, ratiba iliyobadilika ni ya kipindi cha mchana ambapo
sasa Bunge litaanza saa 10:00 jioni badala ya saa 11.00 jioni na
kumalizika saa 12.00 jioni badala ya saa 1.45 usiku.
Amesema mara baada ya kumalizika kwa mfungo huo, ratiba itarudi kama kawaida.
Post A Comment: