Tuesday, 15 May 2018

Benpol afunguka aliwahi kuwa chawa wa BarnabaMsanii wa Muziki wa 'RNB' Benpol anayefanya vizuri na wimbo wake wa 'Natuliza boli' amesema amewahi kuwa chawa wa Barnaba kipindi anaanza safari yake ya muziki.

Benpol amesema hayo katika kipindi cha E-news kinachorushwa na EATV ambapo amemtaja Barnaba kuwa ni msanii ambaye amekuwa msaada kwake wakati anaanza harakati za kuimba muziki na amemsindikiza sehemu nyingi ikiwemo studio.

“Kitu ambacho hamjui mimi na Barnaba urafiki wetu umeanza muda mrefu kwani kupitia yeye nimejifunza vingi na nilikuwa naongozana nae sehemu nyingi kama ambavyo vijana wa leo wanaita ‘chawa’ basi mimi nimewahi kuwa chawa wa Barnaba”. Amesema Benpol

Hivi Karibuni Benpol kupitia ukurasa wake wa Instagram alipost picha ikionesha mazungumzo yake na Barnaba kwa njia ya ‘Videocall’ na kuandika “Was on a video call with my Blood, alikuwa ananiambia kuwa wimbo wetu tulioufanya umekamilika na umekuwa noma sana!!! Love you Bro, Asante sana!! always nice to talk to you”. Aliandika Benpol

No comments:

Post a comment