Tuesday, 29 May 2018

Belle 9 Akana Tetesi za Kukimbia Mjini Baada Ya Kufulia

Msanii mkongwe wa Bongo fleva aliyewahi kutamba na kibao chake cha ‘Masogange’ Belle 9 amekana tetesi zinazodai kuwa amefulia.

Belle 9 alipata shavu la kusainiwa na label ya ‘Vitamin Music’ ambayo ilimuhamisha kutoka Morogoro na kumleta Dar kwa ajili ya kufanya Muziki lakini baada ya kuoa  Belle 9 alipotea kidogo.

Baadae zilizuka stori kuwa Belle 9 ameamua kurudi nyumbani Morogoro kutokana na kukosa shoo na kufulia hapa Dar kiasi ya kwamba ana kosa hata pesa ya kulipia kodi ya nyumba.

Kwenye Interview aliyofanya na Enews ya East Africa Tv, Belle 9 amekana tetesi hizo za kufulia na kusema hajahama Dar bado yupo mjini:

"Dah Hapana muda mrefu sijafika Morogoro mi Nipo Dar, hizo ni rumors tu zinazosambazwa na watu Lakini pia naona wanasema hivyo kwa sababu sionekani Kwenye maeneo ya starehe mengi."

Belle 9 amerudi upya na kazi yake mpya aliyotoa siku chache zilizopita inayokwenda kwa jina la ‘Dada’.

No comments:

Post a comment