Sunday, 27 May 2018

Ajali ya Meli yaua watu zaidi ya 50 DRC

 Watu zaidi ya 50 wameripotiwa kufariki na wengine kadhaa hawajulikani walipo baada ya mtumbwi waliokuwa wakosafiria kuzama nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Ajali hiyo imetokea katika mto Tshuapa Kaskazini Magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. 
Ajali hiyo imetokea Monkoto  kuelekea Mbandaka eneo ambalo kunapatikana janga la virusi vya Ebola tangu May 8.
Watu 50 wameripotiwa kufariki katika jali hiyo. Taarifa kuhusu ajali hiyo imetolewa na  Naibu gavana wa Tshuapa Richard Mboyo Iluka.

No comments:

Post a Comment