Thursday, 26 April 2018

Wema ampiga dongo Mange Kimambi kuhusu maandamano yake

Wema Sepetu amempiga dongo Mange Kimambi kufuatia maandamano aliyokuwa akiyahamasisha kupitia mitandao ya kijamii akiwataka Watanzania waandamane kutokufanikiwa.

Mange alikuwa akiwashawishi Watanzania kuandamana leo katika maadhimisho wa miaka 54 ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni ishara ya kupinga baadhi ya mambo yanayofanywa na serikali ya awamu ya tano, lakini hata hivyo, maandamano hayo hayajafanyika katika kiwango kilichokuwa kikidhaniwa.

Watu wengi leo walikaa majumbani mwao wakihofia kutoka nje kutokana na polisi kutishia kuwashughulikia wale wote watakaoandamana, hali iliyopelekea baadhi ya watu kukatisha shughuli zao.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Wema amesema kuwa alisitisha safari yake ya kwenda Arusha kutokana na hofu kuwa kungekuwa na maandaamano, kumbe hakuna kitu chochote.

“Watu Tukajua Kuna Maandamano mpaka Safari tukazihairisha… Kumbe hamna kitu… Ila utani tuweke pembeni wengi wetu tulishtushwa… But one thing y’all have to understand is Wa Moja Wa Moja tu… Aliepewa kapewa… And Kamwe huwezi shindana na POWER.”

Aliendelea kusema, “ARUSHA… Tunaomba Radhi… We had to Cancel our Trip sababu ya Haya Mambo ya Uongo na Kweli… But Tunakuja Soon tutawajulisha wapendwa wetu.”

Licha ya kuwa Wema hakumtaja Mange katika ‘post’ yake, lakini ni dhahiri kuwa dongo hili limeelekezwa kwa Mange kwani ndiye alikuwa mhamasishaji mkuu wa maandamano haya ambayo Wema amesema ni ya uongo.

A

No comments:

Post a comment