Thursday, 19 April 2018

Walichokisema Diamond na Nandy Baada ya Kuhojiwa TCRA


Wasanii Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Faustina Charles ‘Nandy’ wamehojiwa kwa saa mbili na Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA).

Wakizungumza mara baada ya kumaliza mahojiano hayo yaliyofanyika leo Aprili 19, wasanii hao wamesema wamejifunza mengi kuhusiana na masuala ya mitandao.

Diamond amesema: “Ujana ni maji ya moto tumeelimishwa, hatutarudia tena, nitakuwa balozi kwa vijana wenzangu kuhusu masuala ya mitandao.”

Nandy amesema: “Nisameheni kwa yaliyotokea. Hapa TCRA nimepata somo kuhusu mitandao, tukio lile halitajirudia tena

No comments:

Post a comment