Thursday, 26 April 2018

Uvccm Kata ya Kimandolu watoa msaada katika kituo cha watoto Yatima


Umoja wa Vijana wa ccm  Kata ya  Kimandolu mapema leo Asubuhi  wametoa msaada wa  vitu mbalimbali kama vile Unga, Maharage,Sukari,sabuni za unga, Mafuta ya kula ,chumvi pamoja na vifaa mbalimbali katika kituo cha Kulelea watoto yatima cha "Kindness Orphan"kilichopo katika Kata ya Kimandolu.
Akizungumza mgeni Rasmi katika halfa hiyo  baada ya kukabidhi msaada huo ambaye ni Katibu hamasa wa Umoja wa Vijana Wilaya ya Arusha Mjini amesema 
"Nashukuru sana baadhi ya wadau mbalimbali waliotuwezesha kufanya jambo hili pia niwaombe wadau mbalimbali wasisite kusaidia kituo hiki maana kinalea zaidi ya watoto 40."

No comments:

Post a comment