Rais wa klabu ya Singida United ambaye pia ni mnazi mkubwa wa Yanga, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amesema kuwa mechi yao ya fainali dhidi ya Mtibwa Sugar kombe la Shirikisho la Azam wanaenda kushinda kisha timu za nje watakazo cheza nazo watatumia usafiri wa basi mpaka Singida kwenye uwanja wa Namfua.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba
Waziri, Nchemba ameyasema hayo wakati akihojiwa na kituo cha runinga cha Azam Tv mara baada ya timu ya Singida United kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 2 -1 dhidi ya JKT Tanzania mchezo wa nusu fainali ya kombe la Shirikisho la Azam juzi.
Nashukuru kwamba wameweza kucheza mpira wa burudani na wakitabuni lakini pia wamepata ushindi, kwa maana hiyo yani sisi kwa sasa ni wamajuu tu tunapaa hewani kwapipa kubwa kama la Bombardier  hivi.
Katika kuonyesha kuwa ameyapokea kwa furaha matokeo hayo waziri, Nchemba kama mpenzi wa soka akaleta utani kwa wapinzani wao Mtibwa Sugar ambao maarufu kwa kilimo cha miwa.
Tutakula sukari yote, mashamba yote yamiwa watafyeka wapande alizeti ndicho walichoniambia.
Kwahiyo mimi naamini mechi ya fainali wanaenda kushinda, halafu timu za nje licha ya kucheza majuu lakini mimi nikuwambie sasa watakuja tu na gari mpaka Singida hapa ili waone kwamba Rais Magufuli alishajenga barabara alafu na usalama barabarani utasimamiwa tochi kwa sana tu watakapo kuwa wanakuja Singida huku.
Uwanja wa klabu ya Singida United, Namfua
Klabu ya Singida United imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup – ASFC), baada ya kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 2-1 dhidi ya JKT Tanzania kwenye dimba la Namfua mjini Singida.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: