Sunday, 8 April 2018

MKURUGENZI WA KIWANDA CHA AHAM SHINYANGA AFARIKI KWA AJALI YA GARI


Gari alilokuwa anaendesha marehemu Ahmed Ally Amiri likiwa limetumbukia mtaroni eneo la Ushirika Mjini Shinyanga katika barabara ya Shinyanga kuelekea Mwanza.
Ahmed Ally Amiri enzi za uhai wake
***
Mkurugenzi wa kiwanda cha pamba cha AHAM kilichopo mjini Shinyanga mkoani Shinyanga Ahmed Ally Amiri amefariki dunia baada ya gari aliyokuwa anaendesha kuacha njia na kutumbukia mtaroni katika eneo la Ushirika barabara ya Shinyanga kuelekea Mwanza. 

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, ACP Simon Haule amesema ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo Jumamosi Aprili 7,2018 majira ya saa tisa alfajiri. 

Amesema gari lenye namba za usajili T.529 BHC Toyota Land Cruiser likiendeshwa na Ahmed Ally Amiri likitokea Shinyanga kuelekea Maganzo liliacha njia na kutumbukia mtaroni na kisha kusababisha kifo chake papo hapo. 


Kamanda Haule amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi hivyo kupelekea kushindwa kumudu kukata kona na hivyo kusababisha gari kuingia mtaroni. 

No comments:

Post a comment