Wednesday, 11 April 2018

Mbunge Msigwa Atishia Kujiuzulu Ubunge Kama Itathibitika Katelekeza Mtoto


Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa amejibu tuhuma za kutelekeza mtoto, baada ya picha kuzagaa kwenye mitandao ikimuonyesha mtoto ambaye amefanana naye akitajwa kumtelekeza.

Msigwa amesema kwamba alichokiandika kwenye mitandao ya kijamii anamaanisha hivyo na  anamtaka mwanamke huyo ambaye ametajwa kuwa miongoni mwa walioenda kwa mkuu wa mkoa wa Dar e salaam Paul Makonda kwa kutelekezwa, asiishie hapo tu bali aende hata Bungeni.

“Ilikoanzia imeanzia kwa Jerry Muro ndiye kasambaza hizi habari, kitu ambacho nakijibu hapa amekianzisha Jerry Muro, sasa mimi nasema kama huyo mtu yupo, nimetoa namba zangu na kama sipatikani aje hapa Bungeni”, amesema Peter Msigwa.

Hapo jana Peter Msigwa ameandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa facebook akisema kwamba iwapo kweli mwanamke huyo yupo na akithibitisha ni kweli amemtelekeza, basi yupo tayari kujiuzulu ubunge wake alionao.

No comments:

Post a comment