Friday, 6 April 2018

Matukio katika picha bungeni leo April 6, 2018

Leo April,6 mwaka huu katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limeendelea mjini Dodoma; Hizi ni baadhi ya picha ya yaliyojiri katika bunge hilo.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiwaeleza jambo Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Dkt. Mwigulu Mchemba na Mbunge wa Jimbo la Kilolo Mhe. Venance Mwamoto, wakati wa kikao cha kumi na moja cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Leo Mjini Dodoma
Picha zaidi;

Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Andrew Chenge akiongoza kikao cha kumi na moja cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Leo Mjini Dodoma

Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akimueleza jambo Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Dkt. Mwigulu Mchemba, wakati wa kikao cha kumi na moja cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Leo Mjini Dodoma

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akimueleza jambo Mbunge wa Jimbo la Chemba Mhe. Juma Nkamia, wakati wa kikao cha kumi na moja cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Leo Mjini Dodoma

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akiwaeleza jambo Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango na Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, wakati wa kikao cha kumi na moja cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Leo Mjini Dodoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akiteta jambo na Mbunge wa Jiimbo la Mtama Mhe. Nape Nnauye, wakati wa kikao cha kumi na moja cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Leo Mjini Dodoma

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Josephat Kandege akijibu maswali ya wabunge, wakati wa kikao cha kumi na moja cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Leo Mjini Dodoma.

No comments:

Post a comment