Makamu wa Rais, Samia Suluhu amewataka wananchi kuacha tabia ya kukata mikoko hovyo huku wakiacha kupanda mingine hali aliyosema itaweza kusababisha athari za kimazingira.

Mama Samia amesema hayo wakati wa ziara yake aliyoifanya kwenye bonde la Kizimbani iliyolenga kuangalia maendeleo ya kilimo cha mpunga yanayofanywa na kikundi cha mazingira cha Fuoni Kibondeni.

Amesema mikoko husaidia kuzuia bahari kupanda juu na kuathiri makazi ya watu waishio jirani na kwamba wananchi hao wasipotambua athari hizo kwa sasa kuna  hatari huko mbeleni wakaja kujuta.

Samia amesema ni vyema wananchi wakatambua umuhimu wa kutunza mazingira yanayowazunguka ili kuweza kuepuka athari za kimazingira zikitokea mara zote huharibu miundombinu mbalimbali.

Ndani ya ziara hiyo ambayo ni maalum kwa ajili ya shughuli za Chama pamoja na mambo mengi Makamu wa Rais ambaye pia ni mjumbe wa Kamati kuu ya CCM, anatarajiwa kukagua miradi ya mbalimbali ya chama ipatayo 42. 
Share To:

msumbanews

Post A Comment: