Saturday, 7 April 2018

Madereva wa vyombo vya moto wafungiwa mtambo wa kukatia leseni (TZDLS)Waendesha vyombo vya moto  katika Wilaya ya Tarime mkoani Mara wamefungiwa mtambo wa kukatia leseni (TZDLS) Tanzania Drivers Lincence System TZDLS ili kupunguza kero iliyokuwepo ambapo madereva hao walikuwa wanaipata huduma hiyo Mjini Musoma.

Akithibitisha kufungwa kwa mtambo huo Mjini Tarime Kamanda Mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya, Henry Mwaibambe alisema kuwa huduma hiyo itasaidia kupunguza kero kwa madereva hao.


Mwaibambe alisema huduma hiyo itasaidia kuingizia serikali mapato na pia madereva wengi watapata leseni licha ya kuwa wengi waolikuwa wamepata  mafunzo ya udereva lakini kutokana na mtambo wa leseni kuwa mbali wengi wao walikuwa wanalazimika  kwenda kuchukua leseni hiyo Mjini Musoma.

Kamanda wa Usalama Barabarani Ally Shaali alisema kuwa sheria ya mwaka 1972 ya usalama barabarani sura ya Namba 68 kifungu cha 19 kifungu kidogo cha (1) inamtaka kila mtu anayeendesha chombo cha moto kuwa na leseni hai.

Kwa upande wake Pius Marwa Katibu wa kijiwe cha waendesha pikipiki kilichopo Girango lango la kutokea Stendi ya magari mjini Tarime alisema kuwawanakumbana na changamoto ya kutozwa faini kubwa na polisi pindi wanapokuwa wamepatikana na kosa.

"Tunatozwa kiasi cha shilingi 3,000 kwa kila kosa moja huku tukilinganishwa tozo hiyo na magari  ambapo nauli yetu ya abiria ni shilingi 500, lakini bado wanatuadhibu kosa kama magari bila kujua kuwa magari yanakusanya fedha nyingi kuliko pikipiki tunaomba sheria hiyo irekebishwe," alisema Marwa.

No comments:

Post a comment