Siku chache baada ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, (CAG), Profesa Mussa Assad, kusoma ripoti yake bungeni, mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde amewashukia wabunge wa Chadema bungeni akitumia ripoti ya CAG.

Akizungumza bungeni leo Aprili 13, Lusinde amesema ripoti ya CAG imebainisha kasoro kadhaa ikiwamo madeni hewa na makusanyo yasiyoingizwa kwenye akaunti.

“Ripoti ya CAG ukurasa 266, imebainisha kuwa kuna mkopo ambao haukuthibitishwa mapokeo yake. Agosti 26 Sh866 milioni zililipwa kwa mwanachama kwa niaba ya chama nje ya deni hilo, kwa ajili ya mabango na Sh765 milioni zililipwa kwa mwanachama kama marejesho ya fedha hizo bila kuambatanisha makubaliano ya kisheria,” amesema Lusinde.

Lusinde ameongeza: “Wajinga ndiyo waliwao, mnakalia maandamano, maandamano, mnaacha wenzenu wanapiga hela.”

 Lusinde amedai kuwa ndani ya Chadema kuna ubadhirifu mkubwa na kuwataka Watanzania wajue kuwa, chama hicho kina ufisadi mkubwa.

“Nipigieni makofu kwa ukweli ninaowapa.  Huu ni ukweli mtupu. Ukianza kumulika nyoka, anzia kwenye miguu yako,” alisema.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: