Wednesday, 11 April 2018

Kocha Lwandamina aitosa Yanga SC ajiunga rasmi na Zesco United

Hatimae yametimia, aliyekuwa kocha mkuu wa klabu ya Yanga, George Lwandamina amerejea kwao Zambia na kutangazwa rasmi kujiunga na timu yake ya zamani ya  Zesco United ambayo alikuwa akiifundisha kabla ya kuja nchini kujiunga na miamba hiyo ya Jangwani.
Taarifa rasmi kutoka ndani ya klabu ya Zesco United iliyotolewa hapo jana aprili 10 imemtambulisha rasmi Lwandamina kuwa kocha mkuu akichukua mikoba ya Tenant Chembo.
Aprili 8 mwaka 2018 Zesco United ilitangaza kuachana na aliyekuwa kocha wake Chembo baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Nkana FC.
Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa kupitia mahojiano yake amewahi kusema kuwa hajui lolote kuhusu taarifa hiyo, kama Lwandamina ameondoka basi hajamuaga.

No comments:

Post a comment