Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro amesema Jeshi lake liko
imara kweli kweli katika kupambana na watu wanaotaka kuleta uvunjifu wa
amani nchini, huku akiwasii wanaotaka kuandamana kuacha mara moja kwani
kitakachowapata wasije kulaumiana
IGP
Sirro ametoa kauli hiyo leo (Aprili 7, 2018) wakati akitoa salamu zake
kwa Rais Dkt. Magufuli katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliopo mjini
Arusha baada ya uzinduzi wa nyumba za askari na kushuhudia maonesho ya
utayari ya jeshi hilo katika kukabiliana na uhalifu.
"Mhe.
Rais Magufuli Jeshi lako la Polisi liko imara tena imara kweli kweli,
kwa kupambana na watu wote wanaotaka kuleta uvunjifu wa amani hapa
nchini na kwa bahati nzuri wananchi wapo pamoja na wewe Rais na Jeshi
lako.
"
Ila naomba nitoe ushauri wa bure kwa wale wote wenye nia ya kuchafua
amani ya nchi yetu , ni wasii waache mara moja na kama wataona ushauri
huo hauna maana basi baadae tusilaumiane", amesema IGP Sirro.
Pamoja
na hayo, IGP Sirro ameendelea kwa kusema "upo uhamasishaji kwenye
mitandao, na hili niseme naamini wameshaandamana kwenye mitandao na
wameshamaliza maandamano yao. Kwa hiyo la msingi sana tujenge nchi
yetu".
Kwa
upande mwingine, IGP Sirro amesema katika kipindi cha mwezi Januari
hadi Februari mwaka 2018 kuna jumla ya matukio ya jinai yaliyoripotiwa
ni 96,363 ikilinganishwa na matukio 104,073 yaliyoripotiwa kipindi kama
hicho mwaka 2017.
Post A Comment: