Friday, 6 April 2018

Biliioni 5 Zimetuumika Kujenga Ukuta Madini ya Tanzanite


 Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) Meja Jenerali Martin Busungu amesema gharama za ujenzi wa ukuta wa mgodi wa Tanzanite,  ni Sh5 bilioni.

Jenerali Busungu amesema ukuta huo wenye kilometa 24.4 utazunguka eneo lote la mgodi wa Tanzanite na tathmini ya awali, ilionyesha kwa kilometa 21 zingetumika Sh 4 bilioni.

Akizungumza leo Aprili 6 katika uzinduzi wa ukuta huo, Busungu amesema vikosi 20 vya JKT vimejenga ukuta huo.

“Tumetekeleza kwa uadilifu na uamnifu ujenzi huu. Tunatoa shukran za dhati kwa taasisi za uhandisi Tanzania kwa ushirikiano  wao,” amesema

Amesema Jeshi la JKT lipo tayari kutekeleza maaagizo yoyote yakatayotolewa kwa mustakabali  wa Taifa.

“Hata hivyo kulikuwa na changamoto kadhaa ikiwamo  ugumu wa ujenzi hasa katika miamba, uwepo njia za nyingi za maji ambazo hata hivyo wahandisi  wa Pangani River walisaidia,” amesema

 Leo Rais John Magufuli anazindua ukuta huo.  Viongozi mbalimbali, wakuu wa mikoa, wa wilaya na mawaziri wamehudhuria hafla hiyo.

No comments:

Post a comment