Mkurugenzi wa halmashauri ya Arusha vijijini Dokta Charles Mahera  amewataka wanawake kujikomboa kwa kuwa mstari wa mbele katika kutokomeza  mila potofu zinazowanyima kushiriki katika mipango ya maendeleo pamoja na kupiga vita mimba za utotoni.

Dokta  Mahera amesema  wakati wa maadhimisho ya Siku ya wanawake duniani katika halmashauri hiyo ambapo katika kuhakikisha halmashauri hiyo inakuwa sehemu ya kuwasaidia wanawake kuondokana na Changamoto hiyo ameiagiza  Idara ya ustawi wa jamii kabla ya kufika June mwaka huu  kuhakikisha kamati zinazopinga ukatili kwa wanawake na watoto zinaundwa katika kata zote 27 za halmashauri hiyo.


Hindu Ally Mbwega Mkurugenzi wa kituo cha maendeleo ya wanawake,watoto na Vijana amesema kuwa unyanyasaji wa wanawake na watoto umekuwa ni mwingi kupita kiasi kutokakana na mambo mengi kufanyika kichinichini hasa  maeneo ya pembezoni ikiwa ni pamoja na haki kupotelea mahakamani.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: