Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimedai uchaguzi mdogo katika majimbo ya Kinondoni na Siha uliofanyika Februari 17, 2018 ulikuwa huru, lakini haukuwa wa haki kwa sababu vyama vya upinzani vilionewa.


Akizungumza leo Alhamisi Machi 1, 2018 Kaimu Mkurugenzi wa kituo hicho, Anna Henga amewaeleza waandishi wa habari kuwa kulikuwa na upendeleo kwa CCM, kwamba mawakala wa vyama vya upinzaniwalinyimwa viapo katika vituo vingi na kusababisha vyama hivyo kukosa waangalizi.

"Sisi hatuogopi kuitwa Chadema wala chama kingine cha upinzani kwa sababu tunafuata sheria. Kama uonevu ulikuwepo lazima tuseme," amesema Henga.

"Kulikuwa na uonevu kwa vyama vya upinzani, mawakala wao walinyimwa viapo au kupewa nakala. Tuliwashuhudia mawakala wao wakihangaika kutafuta viapo, wengine walipata saa 8 mchana. Lakini mawakala wa CCM walipewa mapema na walikuwa vituoni."

Henga pia amesema kitendo cha kuwa na idadi kubwa ya  polisi katika vituo vya kupigia kura kiliwatisha wananchi kujitokeza vituoni.

Pia ameeleza jinsi viongozi wa Serikali walivyotumia magari ya umma katika kampeni za uchaguzi huo kwamba haikuwa haki.


Share To:

msumbanews

Post A Comment: