Friday, 23 March 2018

JPM AFANYA UTEUZI WA MKURUGENZI MKUU WA TUME YA NGUVU ZA ATOMIKIRais Dkt. John Magufuli amemteua Prof. Lazaro S.P. Busagala kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC). Kabla ya uteuzi huo Prof. Busagala alikuwa Makamu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) – Taaluma na Utafiti.

Pia, amemteua Prof. Damian Gabagambi kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC). kuchukua nafasi ya Mlingi Elisha Mkucha ambaye atapangiwa kazi nyingine.

No comments:

Post a comment