Wednesday, 14 February 2018

Rais Magufuli atoa kibali cha ajira 52,000

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amempa kibali cha kuajiri watumishi 52,000 katika idara mbalimbali za serikali ikiwemo sekta ya afya.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa eneo la huduma za mama na watoto katika hospitali ya Amana iliyopo Ilala jijini Dar es salaam.
“Serikali inaendelea kuajiri, Rais Magufuli ametupatia kibali cha kuajiri watumishi 52,000 katika idara mbalimbali tayari tulishaanza na Afya lakini tulinza na idadi ndogo,” alisema Waziri Mkuu.
Aidha Waziri Mkuu amesema kuwa Mh. Rais ametoa bilioni 161.9 kwaajili ya kuboresha vituo vyote vya afya, kuboresha Theatre, maabara pamoja nyumba za watumishi.

No comments:

Post a comment