Thursday, 22 February 2018

Picha: Rais wa FIFA, Gianni Infantino awasili nchini rasmi alfajiri ya kuamkia leo


Hatimaye rais wa Shirikisho la mpira wa miguu duniani fifa, Gianni Infantino amewasili nchini majira ya saa 10 : 30 alfajiri ya kuamkia leo na kupokelewa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa JK Nyerere.
Infantino atakuwa hapa nchini kwaajili ya mkutano mkuu wa mwaka wa FIFA unaotarajiwa kuanza leo Februari 22 katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere huku ukitegemewa kuhudhuriwa na wajumbe mbalimbali wa Shirikisho hilo.

Baada ya kuwa hapa nchini, Infantino ataonana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli.

Mkutano huu wa viongozi wa FIFA na CAF umebeba ajenda mbalimbali  ikiwemo kujadili Maendeleo ya Soka la Wanawake, Maendeleo ya Soka la Vijana, Utaratibu wa kusaidia Vilabu vya soka pamoja na vipaumbele mbalimbali vya kukuza soka kwa nchi za Afrika.
Infantino anatarajiwa kuondoka nchini mara baada ya kumaliza mkutano wake na kushiriki chakula cha jioni.

No comments:

Post a comment