Wednesday, 14 February 2018

Mbosso hafikirii kushindana na AslayMsanii wa muziki Bongo, Mbosso amesema mashabiki wanaomchukulia kwamba amekuja kwenye Bongo Flava ili kuleta ushindani kwa Aslay ni mitazamo yao tu.
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na ngoma ‘Watakubali’ amesema anaheshimu kile anachofanya Aslay wale hajafikiria kuja kushindana naye.
“Mimi naheshimu muziki wa Aslay kwa sababu ni mtu ambaye nimemkuta kwenye Industry, halafu kwangu mimi yule ni brother, tunaheshimiana na muheshimu sana,” amesema Mbosso.
Mbosso ambaye hivi karibuni alijiunga rasmi na label ya WCB alikuwa ni miongoni mwa wasanii waliokuwa wakiunda kundi la Yamoto Band kwa kushirikiana na Aslay, Beka na Enock Bella.

No comments:

Post a comment