Nchi ya Afrika Kusini inaendelea kushika headlines kwenye vyombo vya habari vya kimataifa baada ya aliyekuwa Rais wa Nchi hiyo Jacob Zuma kukubali rasmi kujivua urais jana February 14, 2018 baada ya shinikizo kutoka kwa chama tawala cha ANC.

Habari za muda huu kutoka nchini humo ni kwamba Bunge limemteua aliyekuwa Makamu Mkuu wa Rais wa nchi hiyo Cyril Ramaphosa kuwa Rais mpya wa Afrika Kusini na kueleza kuwa ndiye atakuwa kiongozi bora katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi nchini humo.

Zuma alikuwa akikabiliwa na tuhuma nyingi, moja ikiwa ni kumhusisha na vitendo vya rushwa japokuwa mwenyewe amekanusha kuhusishwa na tuhuma hizo. Kutokana na hilo bunge lilipiga kura ya kutokuwa na imani naye na baadaye chama tawala ANC kikamlazimisha kuachia madaraka kwa hiari.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: